Isha Mashauzi aibuka na jipya kuhusu taarabu
Msanii Isha Mashauzi maarufu kama Jike la Simba ameibuka na kusema muziki wa miondoko ya taarabu nchini hauwezi kufa kama baadhi ya watu wanavyodhani, kwa madai wao hawategemei 'kiki' katika kufanya kazi zao kama wanavyofanya wasanii wengine.