Polisi Mwanza wanamshikilia Zumaridi
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limemkamata na linaendelea kumhoji Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi (42), mkazi wa mtaa wa Buguku, Buhongwa mkoani Mwanza, kwa tuhuma za kuendesa shughuli za kidini bila usajili pamoja na kufanya mahubiri kwa waumini wake kwa sauti ya juu.