Afisa Manunuzi awekwa ndani Manyoni
Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amemsweka ndani afisa manunuzi wa halmashauri ya Manyoni Joseph Swila kwa kukiuka maagizo aliyoyatoa jana wakati alipofika kukagua ujenzi wa wodi ya wanawake, wanaume na chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya Manyoni.