Kijana adaiwa kufariki mazingira ya kutatanisha
Jovin Godlove kijana (19) mkazi wa Kijiji cha Nduruma amekutwa ameuawa katika mazingira ya kutatanisha eneo la Njiro jijini Arusha, huku ndugu wa karibu wakisema kijana huyo kabla ya kifo chake alipotea kwa muda wa wiki mbili akiwa na msichana aliyesadikika kuwa ni mpenzi wake.