Achomwa kisu kisa kelele wakati akihubiri injili
Anord Mpobela ambaye ni Mchungaji wa huduma ya Caanan International Ministry, anayehubiri neno la Mungu katika mitaa jiji la Arusha, amechomwa kisu cha kiganja na mtu anayedaiwa kuwa ni raia wa Misri kwa kilichoelezwa kwamba mtu huyo amekuwa akichoshwa na kelele za mhubiri huyo.