Miss Tanzania ataka somo la hedhi mashuleni
Miss Tanzania Mwaka 1998, Basila Mwanukuzi ameishauri serikali kuweka somo la kuwafundisha mabinti namna ya kujihifadhi ngazi ya shule za msingi kwa kupitia walezi (Matron) kipindi wanapokuwa wameanza kupata mabadiliko ya ukuaji wa mwili.