BASATA walia na lugha inayotumika kwenye singeli
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemshauri msanii wa singeli Manfongo, kutumia lugha za misamiati na mafumbo katika kazi zake ili kuepusha maneno ya mtaani ambayo yanatafsirika kwa kuwa muziki huo unasikilizwa na watu wa rika tofauti.