Wananchi wapiga simu kituoni kuwasalimia Polisi
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewaonya baadhi ya wananchi mkoani humo wanaoipiga namba ya dharura ya 114 kwa ajili ya kuwasalimia askari kama mchezo na kuwataka kuitumia namba hiyo pale wanapokuwa wanahitaji msaada wa uokozi pamoja na majanga mengine.