Yanga na Majimaji zasababisha rungu kwa mwamuzi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemwondoa Mwamuzi Hussein Athuman kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu baada ya kupata alama za chini ambazo hazimwezeshi kuendelea tena kuchezesha ligi hiyo.