Utamaduni wa kutopima afya waongeza saratani
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Crispin Kahesa amesema watanzania wengi hawana utamaduni kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini kama kuna dalili zozote za magonjwa ili yaweze kutibiwa mapema.