Semina yatolewa kwa washiriki Tuzo za EATV
East Africa Television Ltd leo imetoa semina kwa wasanii waliofanikiwa kuingia kwenye vipengele tofauti tofauti vya Tuzo za EATV, ikishirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na wadau wengine ambao ni wadhamini wa tuzo hizo.

