TAKUKURU Tanga yaokoa zaidi ya Milioni 76
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuokoa kiasi cha Milioni 76,048,459.1 baada ya kuwafikisha mahakamani waliokuwa watumishi wa umma kwa tuhuma za ubadhirifu na ufujaji wa Fedha za Umma katika wilaya za Kilindi, Korogwe na Tanga Jiji.