Wananchi watakiwa kushiriki uchangiaji elimu
Wananchi wa kata ya Madimba, halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wametakiwa kushiriki kikamilifu zoezi la kufyatua Matofali lililolenga kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu ya elimu zikiwamo nyumba za walimu na vyumba vya madarasa.