Sare na Marekani yampa jeuri Shime mbele ya India.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, Bakari Shime amesema hana wasiwasi kesho atakapowavaa India ambao wenyeji wa michuano maalumu ya soka ya Kimataifa kwa Vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16).