Timu tano hatihati kurejea FDL kuwafuata Coastal
Wakati wadau wakijua wazi kuwa Coastal Union ya Tanga tayari imeaga rasmi Ligi Kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015/16, swali linabaki kwao kwamba ni timu gani itaungana na Wagosi wa Kaya kushuka daraja kutokana na timu tano kuwa katika hatari.