Simba kumwadhibu mtoro Ajib aliye Afrika Kusini.
Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema kamwe hautalifumbia macho sakata la mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib aliyetimkia nchini Afrika Kusini na kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kinyemela bila ruhusa ya klabu hiyo.