Mashali amtwanga Muiran na kutwaa mkanda wa UBO
Kwa mara nyingine mchezo wa masumbwi ya kulipwa nchini umeendelea kuwa nembo ya kuing'arisha nchi katika medani ya Kimataifa mara baada ya jana usiku Mtanzania kutamba mbele ya Muiran na kutwaa mkanda wa dunia wa UBO uzito wa kati kilo 76.4.