Waziri Mkuu kuondoka leo kwenda London
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika Mei 12, mwaka huu.