Trump aishutumu China kubaka uchumi wa Marekani.

Muwania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ameishutumu China kwa kubaka uchumi wa Marekani ikiwa ni mara ya pili mgombea huyo kuishutumu sera ya biashara ya China.

Trump aliuambia mkutano wa wazi huko Indiana kuwa China ilihusika katika wizi mkubwa duniani kwa kubadilisha thamani ya fedha zake ili kufanya biashara ya kusafirisha bidhaa kuwa shindani.

Mara kadhaa Trump amekuwa akiishutumu China kibiashara na kuahidi katika mkutano huo kuwa ataenda kubadilisha jambo hilo na kudai kuwa Marekani ina nguvu zaidi dhidi ya China.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS