Tanzania ya viwanda kutathminiwa.
Wizara ya viwanda na Biashara kwa kushirikiana na shirika la viwanda duniani (NIDO) wameandaa ripoti maalumu ya taarifa itakayoonesha uwezo wa kiushindani wa viwanda vya Tanzania katika kanda na soko la Dunia .
Akiongea na East Africa Radio Mchumi Mwandamizi wa wizara ya viwanda na biashara Bw Valency Mutakyamirwa amesema kuwa ripoti hiyo inayozinduliwac kesho imeangalia jinsi ambavyo Tanzania inaweza kufikia kwenye uchumi wa viwanda kwa kuangalio tuklipotoka , tulipo sasa na tuanapotaka kuelekea kiviwanda.