Nyasi kuwaka moto Taifa leo

Nyasi zinatarajiwa kuwaka moto leo Uwanja wa Taifa, kwenye mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka kati ya Azam FC na Simba.

Azam inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 58 na Simba 57 katika nafasi ya tatu, kwa pamoja zinaifukuzia Yanga katika mbio hizo za ubingwa, ambayo ipo kileleni baada ya kufikisha jumla ya pointi 65 kufuatia ushindi wa jana wa 2-1 dhidi ya Toto Africans mjini Mwanza.

Azam imefanya maandalizi ya nguvu kukabiliana na Wekundu hao wa msimbazi ambao wenyewe walienda kujichimbia visiwani Zanzibar kujiandaa na mtanange huo.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS