Prof. Ndalichako atoa onyo kwa wasimamizi wa elimu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewatahadharisha kuwawajibisha maafisa elimu wa shule za msingi watakaoshindwa kusimamia elimu na kusababisha wanafunzi wamalize shule za msingi bila kujua kusoma na kuandika.