Eneo la Gwale laimarika kwa usafiri wa reli.
Shirika la Reli nchini Tanzania TRL limesema kuwa eneo korofi la Gulwe lililokuwa limeharibika kufuatia mvua zilizokuwa zinanyesha limeshapatiwa ufumbuzi wa kudumu na limeimarika hivyo kuiruhusu treni za abiria na mizigo kuweza kupita bila ya tatizo lolote.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Meneja uhusiano wa TRL Midladjy Maez amesema kuwa wataalam wamefanya ukaguzi wa kina katika eneo la Gulwe na kuthibitisha kuwa limehimarika hivyo ifikapo tarehe moja mei safari zitaanza kama kawaida.