TCRA; Simu bandia zapungua nchini Tanzania.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania, ( TCRA), imesema kuwa takwimu zinaonyesha idadi ya simu bandia zinaendelea kupungua nchini kwa kipindi hiki cha mpito kuelekea kufungwa kwa simu hizo bandia Juni 16 mwaka huu.
Akiongea wakati wa kutoa tathmini ya hali halisi kuelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TCRA), Mhandisi James Kilaba, amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza simu bandia kutokana na elimu inayotolewa kwa jamii kuanzia Desemba mwaka jana ambapo takwimu zilikua asilimia 30 na sasa imefikia asilimia 13.