Fadlu Davids atoa fundisho kwa Makocha Tanzania

Kocha Fadlu Davids yeye ndiye sababu ya timu yake kuongoza msimamo wa ligi msimu huu licha ya kuwa ndio msimu wake wa kwanza kwenye kikosi hiko huku kukiwa na presha kubwa ya kuhitaji kushinda ubingwa wa ligi sambamba na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika kwa ngazi za Vilabu. Kocha huyo raia wa Afrika ya kusini ameijenga timu yake kupata matokeo chanya katika hali yoyote bila kuangalia inachezaje.

Timu ya Simba SC inaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania kwa tofauti ya alama 1 ikiwa na alama 40 ikifuatiwa na Yanga SC yenye alama 39. Kikosi hiko cha Wekundu wa Msimbazi kimekuwa hakichezi soka la kuvutia kama Mashabiki wengi wa Soka Tanzania wangependa kuona timu hiyo ikicheza.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS