Uganda kumalizia uchaguzi leo, UM yaishutumu
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeshutumu serikali ya Uganda kwa kufunga mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi kwa madai ya kuimarisha usalama wa taifa huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki dunia kwenye ghasia zinazohusiana na uchaguzi.