Diarra atakosa michezo ya ligi kuu kuu Tanzania bara pamoja na ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe Januari 3, Al Hilal januari 10, na MC Algers utakaochezwa Januari 17 2025 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Golikipa wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Mali Djigui Diarra atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita akiuguza majeraha ya kigimbi cha mguu na nyama za paja.