Aishi Manula mambo magumu ndani ya Simba SC

Zikiwa zimesalia siku 6 pekee dirisha dogo la usajili Tanzania bara kufungwa Januari 15/2025 ambalo lilifunguliwa Disemba 15/2024, Jina la Aishi Salum Manula mwenye umri wa miaka 29 ni miongoni mwa wachezaji wa Simba Sc ambao hawajapata nafasi ya kucheza chini ya Kocha wa Fadlu Davids kwenye mechi za ushindani msimu huu kutokana na kiwango bora anachoonesha Moussa Camara raia wa Guinea.
Manula ametemwa na Simba kwenye kikosi cha wachezaji 22 waliosafiri kuelekea Nchini Angola kwenye mchezo wa 5 wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos Do Maquis utakaopigwa Januari/12/2025.