Bukoba waomba Soko la kisasa na kituo cha mabasi
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameishauri serikali kutafuta eneo jipya kwa ajili ya ujenzi wa soko kubwa na la kisasa na kukamilisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi ambacho ujenzi wake umeanza katika eneo la Kyakailabwa, lengo likiwa ni kufungua fursa za kiuchumi