Real Madrid mambo magumu klabu bingwa Ulaya

Kipigo hiko kutoka kwa Liverpool kwenye uwanja wa Anfield kumeifanya Madrid kusalia na alama zake 6 baada ya kucheza michezo mitano inashika nafasi ya 24 katika mashindano yenye timu 36. Kikosi cha Los Blancos ndio mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani msimu huu inakutana na wakati mgumu kutokana na kutokuwa kwenye kiwango chake kilichozoeleka katika mashindano ya msimu huu wenye mfumo tofauti na uliozoeleka

Kikosi cha Real FC Madrid siku ya jana kilijikuta kwenye wakati mgumu lilipocheza na timu ya Liverpool ya Uingereza katika mwendelezo wa michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kupoteza mchezo huo kwa magoli 2-0 magoli yaliyofungwa na Alexis Mac Allister na Cody Gakpo.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS