Serikali kumwaga tena mikopo kwa wasanii
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dokta Hassani Abbas wametembelea ofisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa jijini Dar es Salaam na kufanya kikao kazi na watumishi wa mfuko huo.