Fadlu Davies anapaswa kuwa na kikosi cha kwanza

Fadlu Davies anapaswa kubadilika kwenye hili hakuna anayehoji sababu Simba inaondoka na matokeo ya ushindi ila ikatokea inaanza kudondosha alama huku akiwa anaendelea kufanya mzunguko wa kikosi chake atajikuta matatani kwani Mashabiki wataanza kuhoji na presha ikishakuwa kubwa hupelekea viongozi kuchukua hatua ya kumfuta kazi Mwalimu. Timu zote zinazochukua ubingwa huwa zinavikosi vya kwanza walau kwa asilimia 75 mpaka 80 ya Wachezaji walewale kucheza pamoja kwa muda mrefu.
Klabu ya Simba siku ya jana ilipata ushindi wake wa kwanza wa katika kombe la shirikisho mchezo wa kwanza kundi A dhidi ya FC Bravos Do Maquis kutoka nchini Angola. Goli la Jean Charles Ahoua lilitosha kuipa alama 3 muhimu klabu yake mchezo uliopigwa uwanja Benjamini Mkapa Dar es salaam.