Polisi waua majambazi waliokuwa na mabomu
Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, na kufanikiwa kupata bunduki moja aina ya AK47 ikiwa na magazine moja yenye risasi 25 na mabomu mawili ya kutupwa kwa mkono,katika barabara itokayo Kumnazi kuelekea Rulenge wilayani Ngara