Mwanafunzi afariki akidaiwa kupigwa na Mwalimu
Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Sabasaba, Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara, Amina Ally, (16), anadaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kushindwa kujibu swali darasani, na kupelekea kudondoka na kupoteza fahamu akiwa shuleni hapo.