Simba SC kukipiga dhidi ya F.C. Bravos do Maquis

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinajivunia historia nzuri kinapocheza uwanja wake wa nyumbani katika mashindano ya vilabu Afrika kombe la shirikisho na klabu bingwa. Katika mashindano haya ya shirikisho Simba SC imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali msimu wa 2020-2021 ambapo iliondoshwa mashindanoni na timu ya Kaizer Chiefs kutokea Afrika ya kusini.
Klabu ya Simba itacheza mchezo wa kwanza kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya F.C. Bravos do Maquis kutokea Angola kesho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.