Waliovamia msitu wa Kuni watakiwa kuondoka
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewataka wananchi waliovamia hifadhi ya msitu wa Kuni wilayani Mvomero mkoani Morogoro na kuanzisha shughuli za ujenzi wa nyumba katika hifadhi hiyo wasitishe na kuondoka mara moja katika eneo hilo ili kulinda ikolojia ya eneo.