Sead Ramovic kuanza kibarua dhidi ya Al-Hilal

Malengo ya timu ya Wanajangwani ni kufika nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika na safari yao itaanza kesho dhidi ya Al-Hilal S.C ambayo si timu nyepesi kutokana na historia ya timu hiyo katika mashindano ya vilabu ya CAF.Yanga SC itaingia kwenye mchezo huu ikikumbuka msimu wa 2021-2022 ambapo iliondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa dhidi ya mpinzani wake wa kesho.

Kocha mkuu mpya wa klabu ya Yanga Sead Ramovic anatarajiwa kuanza kibarua chake rasmi kesho atakapoiongoza tmu yake dhidi ya Al-Hilal S.C. kutokea nchini Sudani mchezo wa makundi mzunguko wa kwanza utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS