Ukosefu wa Mawasiliano wachelewesha matokeo Mtwara
Ukosefu wa mawasiliano katika baadhi ya maeneo mkoani Mtwara imetajwa kuwa ndio sababu iliyochangia ucheleweshaji wa kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni za uchaguzi kwa wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani.
Hayo yamezungumzwa jana na katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo, Shaibu Akwilombe, alipokuwa akitangaza matokeo ya awali ya majimbo sita kati ya tisa yaliyofanya uchaguzi.