"Sichukii mkiniita Bi tozo" - Rais Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba wala halichukii hata kidogo jina alilopewa la 'Bi tozo' na kwamba serikali itaendelea kutoza kodi na tozo kwa lengo la kuleta maendeleo kwa Watanzania.