Moalin Mkurugenzi mpya wa ufundi Yanga SC

Nafasi ya Ukurugenzi wa ufundi ni nafasi nyeti sana kwenye timu kwani mipango ya timu kuanzia falsafa ya timu aina ya uchezaji wa timu Wachezaji wanaohitajika na timu kulingana na aina ya falsafa iliyopo kwa wakati huo, mipango ya baadae aina gani ya Kocha aajiriwe yote ipo chini ya utendaji wa Mkurugenzi wa ufundi.
Aliyekuwa Kocha mkuu wa timu ya KMC FC ya Dar es salaam Abdihamid Moalin ametangazwa na klabu ya Yanga kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo leo mchana.Utambulisho huo umemaliza yale mazungumzo ya chinichini kuhusiana na wapi atafanya kazi Kocha huyo baada ya kuondoka KMC FC.