Aliyeripotiwa amepotea akutwa mochwari M/Nyamala
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa Daisle Simion Ulomi, aliyekuwa ameripotiwa kwamba amepotea, alifariki dunia baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia siku ya Desemba 11, 2024.