Cleveland Cavaliers yazidi kung'aa NBA

Huu ni mwanzo bora wa ligi ya kikapu Marekani NBA tangu msimu wa 2015-16 klabu ya Golden State Warriors iliyocheza michezo 24 mfululizo kwenye msimu huo.Donovan Mitchell amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu kwa Cavaliers kamaliza mchezo wa jana akiwa amefunga alama 36 na Wachezaji wengine watano wamefikisha alama zaidi ya kumi mchezo wa jana huku ikitoka nyuma kwa alama 9 robo ya tatu na kushinda mchezo huo.
Cleveland Cavaliers yazidi kung'aa NBA baada ya jana kushinda mchezo wake wa 12 mfululizo dhidi ya Chicago Bulls kwa vikapu 119-113.