Majeruhi yamchanganya Ancelotti Madrid

Ushindi wa goli nne kwa sifuri dhidi Osasuna mchezo uliopigwa uwanja wa Santiago Bernabéu Stadium siku ya Jumamosi ya Novemba 9 mchezo huo ulitamatika huku kukiwa na majeruhi wapya kwa kikosi cha mabingwa watetezi wa La liga, Eder Militao atakaa nje ya uwanja miezi 9 baada ya kuumia goti,  Rodrygo Goes na Lucas Vazquez wote walipata majeraha kwenye mchezo huo.

Kocha wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Carlo Ancelotti anapitia wakati mgumu ndani ya Madrid kutokana na kuongezeka kwa idadi ya majeruhi kwenye kikosi chake.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS