SUA wampa tuzo Jafo kwa kuleta tija kwenye jamii
Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimetoa tuzo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo kwa kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wakati akiwa mwanafunzi chuoni hapo.