Tanzania itapunguza vikwazo vya barabarani: JK
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa kuna haja ya kuhakikisha kuwa uendelezaji na uwekezaji katika nchi za ukanda wa Kati wa miundombinu na maendeleo, unalenga pia katika kuboresha ustawi wa maisha ya raia wa nchi hizo.