Wananchi waililia serikali nyumba zao kubomolewa
Wamiliki wa nyumba 14 zilizopo katika kitongoji cha Sokoni Kijiji cha Kahunda halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, wameiomba serikali isitishe zoezi la kubomoa nyumba zao linaloendeshwa na serikali ya Kijiji hicho kwa madai kuwa hawakushirikishwa kuhusu zoezi hilo.