Watanzania 80% kupata elimu ya fedha ifikapo 2025.
Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha na Mipango ya Tanzania Dkt. Charles Mwamaja amesema kwamba serikali inapanga kuelimisha asilimia 80 ya watu ili kufahamu maswala ya fedha ifikapo 2025 kupitia utekelezaji wa mpango wa elimu ya kifedha.