Takwimu za mechi mbili walizokutana zinaonyesha timu ya Wananchi imeshinda michezo yote miwili dhidi ya Wapinzani wao siku ya leo (3-0, 1-0) Tabora United kutokea Tabora ambayo inashika nafasi ya 10 ikiwa imevuna alama 14 msimu huu.
Kikosi cha Yanga Sc kitashuka dimbani leo kucheza mchezo wa kumi Ligi Kuu soka Tanzania bara leo dhidi ya Tabora United Uwanja wa Azam Complex Chamazi majira ya Saa kumi na mbili za jioni