Makocha watabiri mchezo mgumu Simba SC VS KMC FC

Simba SC itacheza dhidi ya KMC Jumatano Novemba 6,2024 katika uwanja wa Kmc Mwenge, Dar es salaam. Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinashika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzani bara kikiwa kimejikusanyia alama 22 katika michezo 9 huku KMC ikiwa nafasi ya 6 imekusanya alama 14 katika michezo 10.

Makocha wa Simba SC na KMC wameongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo utakaoziktanisha timu zao siku ya kesho Novemba 6 kwenye uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam. Wakufunzi hao wamezungumzia kuhusiana na maandalizi ya timu zao kabla ya kukutana uwanjani kesho.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS