Jose Mourinho aanza utukutu nchini Uturuki

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea FC, Manchester United na Tottenham Hotspurs anasifika kwa uwezo wa kushinda ubingwa na timu zake zote alizowahi kuzifundisha anatumainiwa na Mashabiki wa Fenerbahçe SK kurudisha furaha yao kwa kushinda ubingwa wa Super Lig muda mrefu kwa klabu hiyo umepita bila kushinda ubingwa wa nchi hiyo.
Kocha mwenye maneno mengi barani Ulaya anayefundisha klabu ya Fenerbahçe SK amembwatukia Refarii aliyechezesha mchezo kati ya Sivasspor dhidi ya kikosi cha Mourinho ambao ulimalizika kwa kikosi cha Fenerbahçe SK kuondoka na ushindi wa goli 2-3.